Malkia wa Talk Show, Oprah Winfrey ambaye hivi karibuni alikuwa amepokea maombi ya mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump akiomba awe mgombea mwenza wake, amerudisha majibu husika kwa mgombea huyo mwenye kauli ‘tata’.

Trump alimuomba Oprah kuungana naye kutafuta nafasi ya kuingia ikulu akisisitiza kuwa akiwa naye lazima watashinda kiulaini.

Akifanya mahojiano na Jimmy Kimmel katika show ya Jimmy Kimmel Live, Oprah amemjibu Trump kuwa yeye yuko na Hillary Clinton, mgombea wa Democratic.

“Hiki ni kipindi cha nguvu ya maendeleo yatakayoletwa na wanawake. Kila kitu kinawezekana kama utakuwa kiongozi wa dunia huru. Niko naye (Hillary Clinton),” alisema.

Oprah alizungumzia pia tetesi zilizosambaa kuwa huenda akajiunga kugombea nafasi ya juu ya kisiasa nchini humo na kueleza kuwa hivi sasa hana mpango huo lakini amebaini kuwa kama angetaka kuingia kwenye mchakato huo mwaka huu angekuwa amefaulu kupita kiasi.

Mbatia alina na adhabu za Bunge kwa wapinzani, amtupia lawama Dk. Tulia
Video: CUF yamtaka Profesa Lipumba asikiyumbishe Chama