Mbwa anayeaminika kuwa kichaa ameripotiwa kupenya katikati ya umati na kumvamia polisi wa kupambana na ujambazi katika eneo la Yola nchini Nigeria.

Polisi huyo alijeruhiwa vibaya na ‘jibwa’ hilo kwenye mguu wake wa kulia kabla ya wananchi waliokuwa eneo hilo kumshambulia mnyama huyo na kufanikiwa kumuua kikatili.

Hata hivyo, baada ya kumuua mbwa huyo, umati huo ulipigwa na butwaa baada ya kushuhudia kilichotokea wakati wakisubiri jeshi la polisi kuuondoa mzoga huo.

Shuhuda wa tukio aliyejitambulisha kwa jina la Tizhe Joseph, aliuambia mtandao wa Vanguard kuwa mzoga huo uliokuwa ukisubiri kubebwa na wana usalama uligeuka ‘dili’ kwa watu ambao wanaaminika kuwa hutumia mizoga hiyo kama kitoweo.

“Mtu mmoja anayeaminika kuwa ni mla mbwa alipenya katikati ya umati akaubeba mzoga huo haraka na kutokomea nao huku watu wakibaki na mshtuko,” Joseph alisema.

 

Serikali Ya Magufuli kusambaza madaktari Bingwa 'Pembezoni'
Kubenea aibuka na siku 200 za Lowassa...