Uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli wa kumteua aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro kuwa mkuu wa jeshi hilo nchini umepokelewa kwa shangwe kubwa mkoani Pwani.
 
Aidha, wakazi wa Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji wamesema kuwa iwapo anataka kukomesha mauaji hayo yanayoendelea basi apange mkakati utakaowashirikisha wananchi wa maeneo hayo katika kulishughulikiwa suala hilo.
 
“Uzoefu wa IGP Sirro wa kupambana na waharifu utaweza kutatua tatizo hili kwani amekuwa na mbinu ambazo zimekuwa zikimsaidia kuwakamata wahalifu ama kutatua tatizo ambalo limekuwa sugu,”amesema mzee mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake

Ronaldo aonyesha ubora wake UEFA
Real Madrid watwaa ubingwa UEFA