Mwenyekiti serikali ya Mtaa wa Itulike Kata ya Ramadhani halmashauri ya Mji wa Njombe, Michael Ng’ande amekutana na wananchi wa Mtaa huo na kufanya mkutano wa pamoja kujadili namna ya kuboresha kiwango cha Elimu katika Shule ya Msingi Itulike.

Akizungumza na Wananchi hao, Ng’ande amesema kuwa Shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya Utoro wa wanafunzi ambao kwa asilimia kubwa imetajwa kusababishwa na wazazi wa wanafunzi hao.

Amesema kuwa tatizo hilo la utoro wa wanafunzi limesababisha shule hiyo kufanya vibaya katika matokeo yake kuanzia ngazi ya wilaya na mkoa wa Njombe huku akiwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya msingi Itulike kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha vijana wao wanashiriki masomo kikamilifu.

“Wananchi naomba niseme wazi kuwa walikuja hapa viongozi mbalimbali pamoja na kamati ya Shule na wananchi tuliitwa pale shuleni, kwanza taaluma imeshuka, watoto wengi ni watoro, wengine ni wachafu yaani hali zao ni mbaya, ambapo tatizo kubwa ni sisi wazazi tunaoishi na hawa watoto nyumbani ndio maana tumekutana hapa ili kujadili tatizo hili,” amesema Ng’ande

Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe ameshiriki mkutano huo na wananchi wengine na kutumia fursa hiyo kuwataka wazazi kuhakikisha wana wasimamia watoto wao ili washiriki masomo.

  • Yanayojiri katika ziara ya Rais Magufuli mkoani Mtwara
  • Wahamiaji 12 wakamatwa mkoani Njombe
  • LIVE: Ziara ya Rais Magufuli mkoani Ruvuma

 

Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 2 mkoani Njombe
Wahamiaji 12 wakamatwa mkoani Njombe