Klabu ya Borussia Dortmund imeamua kumuweka nje kwa muda usiojulikana mshambuliaji wao tegemezi kutoka Gabon Pierre Aubameyang kwa kile kilichotajwa kama utovu wa nidhamu.

Katika taarifa rasmi kutoka ndani ya klabu hiyo imethibitisha kuwa Aubameyang hatakuwepo katika mchezo ambao Borussia Dortmund watakapoikabili Stuttgart kutokana na matatizo hayo.

Aidha, hii sio mara ya kwanza kwa Mchezaji huyo kupewa adhabu kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu ambapo mwaka jana mwezi wa 11 aliachwa katika kikosi cha Dortmund kilichocheza dhidi ya Sporting katika mashindano ya Champions League.

Hata hivyo, matatizo kati ya Dortmund na Aubameyang yanaweza kuwa ishara kwamba mwanasoka huyo yuko mbioni kuachana na klabu hiyo kwani kila dirisha la usajili amekuwa akihusishwa na kuikimbia Dortmund.

Katika msimu huu Aubameyang amefunga jumla ya mabao 10 lakini hajawahi kufunga tangu alipofunga katika mchezo dhidi ya RB Leizpg  mwezi October ambapo Borussia Dortmund walifungwa bao 3 kwa 2.

Balozi afunguka alivyomsafirisha 'kijasusi' Dkt. Shika
Sakata la Kakolanya kuidai Yanga lachukua sura mpya