Tetemeko lililokuwa na ukubwa wa 6.7 katika kipimo cha Richa limetokea Elazig, Mashariki mwa Uturuki na kusababisha vifo vya watu 19 na kuwajeruhi watu wengine zaidi ya 300.

Imeelezwa kuwa majengo mengi yameharibiwa kutokana na tetemeko hilo linaloelezwa kuwa na Kina cha Kilometa 10 kwa mujibu wa Shirika la Kijiolojia ambapo Watu takriban 500,000 walilisikia tetemeko hilo.

Aidha, matetemeko 15 baada ya tetemeko hilo kuu yamesikika pia katika Mataifa Jirani kama Iraq, Syria na Lebanon.

Taarifa iliyotolewa na Shirika linalohusika na kutoa huduma ya kwanza katika Matukio ya Dharura (AFAD) imefahamisha kuwa idadi hiyo ya waliofariki inaweza kuongezeka.

KCMC yatengeneza hewa ya kuhifadhi mbegu za uzazi
Video: JPM ahofia kung'olewa Urais, Prof. Kabudi atoboa siri ya kunusurika