Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Iringa umepata Mwenyekiti mpya baada ya kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wa umoja huo Kenani Kihongosi kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Arusha mkoa Arusha.

Katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Ihemi uliopo wilaya ya Iringa, wajumbe wa baraza hilo walipiga jumla ya kura 183 na kuthibisha kuwa Anold Mvamba amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya umoja wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti, msimamizi wa uchaguzi huo mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa MNEC wa Njombe, Fidelis Lumato amemtangaza Anold  Mvamba kuwa ndiye Mwenyekiti mpya baada ya kupata jumla ya kura 18 kutoka kwa wajumbe wote wa umoja huo.

Amesema kuwa jumla ya kura 329 zilipigwa na hakuna kura halali zilizoharibika hivyo mshindi wa kwanza Anord Mvamba amepata 181 na mshindi wa pili Fatma Rembo amepata 123 huku wa tatu Isack Mgovano amepata kura 25.

Alimalizia kwa kuwaomba vijana wote wa umoja huo kuvunja makundi yote waliyokuwa nayo na kuanza kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kuijenga jumuiya hiyo kuwa imara kama ilivyokuwa awali.

Baada ya ushindi huo, Mwenyekiti mpya wa UVCCM Iringa, Mvamba amesema kuwa ataendeleza maono ya Mwenyekiti mstaafu ya kuhakikisha vijana wanakuwa na umoja na mshikamano huku akiwataka vijana kuvunja makundi yote yaliyotokana na uchaguzi ili kuhakikisha wanakijenga chama na kutafuta fursa mbalimbali zitakazowainua kiuchumi.

Awali akitoa nasaa zake kwenye Mkutano Mkuu maalum wa uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Mwenyekiti mstaafu wa UVCCM mkoani humo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi amesema kuwa ili kuwa na jumuiya ya vijana bora ambayo itapika vilivyo viongozi bora, ni lazima kuhakikisha wanaendeleza ushirikiano uliokuwepo kwa viongozi wa chama na serikali.

Kihongosi amesema kuwa kiongozi wa Umoja wa vijana akiendekeza majungu, makundi na mpenda rushwa hawezi kuwa kiongozi bora kwenye kuimarisha umoja wa vijana ambao ndio tanuri la kuwapika viongozi bora.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 13, 2021
Bunge lasimama dakika 20 sakata la malori