Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Raymond Mwangwala amesema kuwa umoja huo unatarajia kuwa wakala wa kutafuta ajira kwa vijana ili kukabiliana na malalamiko ya ajira hasa kwa vijana nchini.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa programu hiyo itahusisha vijana zaidi ya mia tatu nchi nzima ambao watapatiwa mafunzo maalumu na ujuzi mbalimbali ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kutumia sekta mbalimbali za kiuchumi.

“Tuna malengo mengi tunayotaka tuyafanye ikiwemo kuangalia ajira kwa vijana, program ya vijana 300, nikuangalia wana ajirika kwa namna gani, kuna makampuni tumeongea nayo na wako tayari tusambaze ajira zao, kwa hiyo lazima uwe na vijana ambao unajua wana sifa gani.”amesema Mwangwala

Aidha, amesema kuwa kauli mbiu imeanza kipindi hiki cha mabadiliko, hivyo ni lazima waje na vitu vipya, ndio maana wamekuja  na kauli mbiu na CCM mpya, ikiwa na lengo la kujenga ari mpya kwa wanachama. ndio maana imekuwa CCM inayotekeleza, sio ya propaganda na slogani huwa zinabadilika kulingana na wakati.

Akizungumzia BAVICHA, amesema kuwa baraza hilo limekuwa halijihusishi na masuala ya kiuchumi, bali wamejikita zaidi kwenye masuala ya matukio yanayotokea.

 

TPA yawataka Wahandisi kuchangamkia fursa
Watoto wa chekechea wajeruhiwa vibaya na kisu