Siku moja baada ya mwanadiplomasia, Balozi Juma Mwapachu kutangaza kurejea kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM), Umoja wa Vijana wa CCCM (UVCCM) wilayani Hai umepinga kupokelewa kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo, Arnold Swai alisema kuwa ni kosa kubwa kumpokea Balozi Mwapachu kwakuwa ana dhambi ya usaliti ambayo haiponi tofauti na yaliyopita ambayo alidai ni maradhi yasiyoua (si ndwele).

Alisema kuwa Balozi Mwapachu ni moja kati ya wasaliti wa chama hicho aliyekibeza wakati wa mapambano lakini siku chache baada ya kutulia na kusimama imara, amerudi na kutaka yalipita yasiwe maradhi ya kuua (ndwele).

“Ni lazima tujiulize, hivi mwanadiplomasia huyo angekuwa tayari kurejea CCM kama mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa angeshinda urais?,” Balozi Mwapachu anakaririwa.

“Hatuwezi kumpokea msaliti kama huyu, wakati chama kilipokuwa kwenye mapambano aliondoka tena kwa kejeli, leo chama chetu kimesimama imara chini ya mwenyekiti wetu Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ndio anarudi na wimbo uleule kwamba chama kimemlea, haikubaliki,” aliongeza.

Swai alikitaka chama hicho kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote ambao walikubali na kumpokea Balozi Mwapachu.

Juzi, Balozi Mwapachu alirejea CCM na kukabidhiwa kadi kwenye ofisi za chama hicho zilizoko Mikocheni jijini Dar es Salaam ikiwa ni takribani miezi 6 tangu alipotangaza kujiondoa kwenye chama hicho Oktoba mwaka jana kwa madai kuwa kimepoteza muelekeo.

 

 

Miraj Adam Kuwakosa Simba Kesho Mkwakwani
Sports Club Villa Hawakufanya Mazoezi Aman Stadium