Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), Shaka Hamudu Shaka amejibu mashambilio ya Baraza la Vijana Chadema, (BAVICHA) juu ya Rais Magufuli na Serikali ya awamu ya tano baada ya kushambuliwa na Chama Pinzani cha Chadema kufuatia na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edawrd Ngoyai Lowassa kufanya naye mazungumzo Ikulu.

Shaka amewaambia Bavicha kuwa wao kama vijana wa chama tawala CCM, wataendelea kumlinda na kumtetea Magufuli dhidi ya kejeli, dhihaka na kebehi ambazo amekuwa akifanyiwa na upinzani kwa lengo la kutaka kumuondolea heshima ya chama cha mapinduzi.

Hata hivyo Shaka amewaonya na kusema wakiendelea na upuuzi huo wa kukejeli na kukebehi kazi nzuri za Rais na Serikali ya awamu ya tano, wao kama vijana wa CCM wameahidi kuwashughulikia kwani anaamini kuwa  uwezo huo wanao.

Aidha ametoa ushauri kwa Bavicha kua wakae chini na Mwenyekiti wao washauriane jinsi ya kukinusuru chama hicho na kifo.

‘’Chama chao sasa kimekuwa kikichungulia kaburi, kimepoteza mwelekeo na hawaoni kesho yao kisiasa’’ amesema Shaka.

Ameongezea kuwa kwa kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano wapo mbioni kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na 2020 wakiwa hawana Upinzani bali ni mfano wa upinzani kutokana na kupoteza mweleko wa kisiasa.

 

Video: Mbowe atuliza mzuka Chadema, Siri mkataba wa Airtel yafichuka
Mvua yaleta maafa Dodoma