Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa uamuzi wa kutengua uteuzi wa Jokate Mwegelo aliyekuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chupukizi unatokana na kukaimu nafasi hiyo kwa mwaka mmoja bila kuthibitishwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa umoja huo, Shaka Hamdu Shaka ametoa sababu hizo saa chache baada ya Kamati ya Utendaji kupitisha uamuzi huo dhidi ya Jokate.

“Alikuwa anakaimu na hakuwa amethibitishwa kuwa mkuu wa idara kwa kipindi chote cha mwaka mmoja. Mara nyingi ukikaimu ni sawa na kusema upo kwenye majaribio,” alisema Shaka.

Aliongeza kuwa Kamati ya Utendaji ndiyo iliyomkaimisha nafasi hiyo na ndiyo iliyoamua kutengua, hivyo wanazo sababu zao za msingi.

Aidha, Shaka alisema kuwa nafasi hiyo itajazwa baada ya kukamilika kwa taratibu za kikanuni na mamlaka husika kufanya uamuzi kupitia vikao vyake.

Jokate amekaimu nafasi hiyo tangu Aprili mwaka jana alipoteuliwa. Uteuzi wake ulizua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama waliodai taratibu hazikufuatwa ipasavyo.

Boko Haram wawaonya wasichana waliowaachia kutorudi shule
Video: Jokate atenguliwa uongozi UVCCM, Askofu Shoo asema kanisa halitazibwa mdomo