Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, na kituo cha Marekani cha kudhibiti magonjwa CDC wametoa ripoti inaonyesha kuwa ugonjwa wa surua ni tishio duniani kote na kwamba utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo umepungua kwa kasi tangu kuanza kwa janga la Uviko-19.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa, mwaka 2021 rekodi ya juu ya watoto karibu milioni 40 walikosa chanjo chanjo ya surua, ambapo watoto milioni 25 walikosa dozi yao ya kwanza na watoto milioni 14.7 walikosa dozi yao ya pili.

Mtoto akipata matone katika kituo cha Afya. Picha ya SciDev.Net

Aidha, imearifu kuwa kupungua kwa kasi ya chanjo ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya kimataifa, kufikia na kukomesha kabisa ugonjwa wa surua na hivyo kuwaacha mamilioni ya watoto wakiwa katika hatari ya kuambukizwa.

Zaidi ya nchi 20 zilikumbwa na milipuko wa surua na kwamba ni asilimia 81 pekee ya watoto ndio wanaopokea chanjo ya kwanza ya surua, na ni asilimia 71 tu ya watoto wanaopokea chanjo ya pili ya surua na bado idadi inaweza kuongezeka kutokana na milipuko inayoendelea.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 25, 2022 
Benki kuu yaonya kampuni za mikopo