Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria umechangisha dola bilioni 14.25 wakati wa mkutano wa wafadhili uliohudhuriwa na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, huku miongo kadhaa ya maendeleo dhidi ya magonjwa ikirudishwa nyuma na Uviko-19.

Macron ambaye alikuwa akizungumza na viongozi kutoka Marekani, Japan, Ujerumani, Kanada na EU, katika Mkutano wa Saba wa ushirikiano wa afya ya umma, ametangaza ahadi mpya za kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Amesema, “Ushindi dhidi ya janga kubwa ni ndani ya uwezo wetu, lakini bado tuna safari ndefu kwani Watu milioni 38.4 bado wanaishi na UKIMWI, na magonjwa ya malaria na kifua kikuu yanaongezeka katika Afrika, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kusini.”

Mhudumu wa afya akimpatia huduma mgonjwa. Picha na WHO.

Marcon ameongeza kuwa, “Tuna mengi ya kufanya katika miaka ijayo na mwaka 2030 lazima tutimize ahadi yetu, VVU, malaria na kifua kikuu lazima viondoke na nina furaha kutangaza kwamba tutatenga euro milioni 300 za ziada kwa Mfuko wa Kimataifa kwa miaka mitatu, tukiwekeza karibu euro bilioni 1.6 kati ya 2023 na 2025.”

Kiongozi huyo wa Ufaransa, pia aliapa kuendeleza mapambano ya kupunguza bei ya dawa kwa kuwekeza euro milioni 250 kwa miaka mitatu, katika shirika la kimataifa la ununuzi wa dawa la Unitaid.

Tangu Mfuko wa Kimataifa ulipoundwa mwaka wa 2002, umeokoa maisha ya watu milioni 50 na kupunguza kiwango cha vifo vyote kutokana na VVU, kifua kikuu na malaria katika nchi ambazo hazina hiyo inawekeza huku kiwango cha vifo vya kifua kikuu kikipungua kwa asilimia 21 na malaria kwa asilimia 26.

Fiston Mayele: Tutaishangaza Afrika
Juma Mgunda atembelea Coastal Union, awatakia kheri