Ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO), inasema janga la Uviko-19 lilipunguza kasi na juhudi za kudhibiti ugonjwa wa Malaria, na hivyo kusababisha vifo vya ziada 63,000 na maambukizo zaidi milioni 13 ulimwenguni kwa miaka miwili.

Ripoti hiyo, iliyochapishwa hapojana Alhamisi ya Desemba 8, 2022, imesema kesi za ugonjwa huo ziliongezeka zaidi mwaka 2020 na kuendelea kuongezeka kwa kiwango cha chini mapema mwaka 2021.

Aidha, WHO imefafanua kuwa, miongoni mwa changamoto hizo ni spishi mpya ya mbu wanaostahimili viuatilifu vingi, lakini hata hivyo kikwazo kikubwa zaidi bado ni kukosekana kwa ufadhili.

Hata hivyo, Bara la Afrika ndili lililoathiriwa zaidi na malaria huku Umoja wa Mataifa ukisema kwa mwaka jana kulikuwa na vifo 619,000 vilivyotokana na malaria na wastani wa maambukizi milioni 247.

Ya kale Dhahabu: Reli ya zaidi ya karne moja yaokoa usafirishaji
EACP Wakutana kujadili umasikini, maendeleo