Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kesho tarehe 30 Aprili 2021 itatangaza Uwanja utakaopigwa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo ipo kwenye hatua ya robo fainali kwa sasa.

Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa Julai, 2021 kutokana na kuchelewa kuanza kwa michuano hiyo kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

Shughuli za kutangaza Uwanja huo itafanyika kesho katika droo ya kupanga michezo ya hatua ya robo na nusu fainali ya michuano hiyo kwenye makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo Cairo, Misri.

Moja ya kiwanja kinachopewa nafasi kubwa ya kuchezewa mchezo huo wa fainali ni Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam ambao unawezo wa kubeba watazamaji 60,000.

Katika droo hiyo klabu ya Simba itajua mpinzani wake kwenye hatua ya robo fainali mara baada ya kumaliza kinara kwenye kundi A, wakiwa na pointi 13.

Simba huenda akacheza kati ya MC Alger, CR Belouzidad zote kutoka Algeria au Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini.

Timu zote hizo zimeshika nafasi ya pili kwenye makundi yao hivyo lazima wakutane na vinara waliomaliza kwenye makundi mengine.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 30, 2021
Halmashauri kuu ya CCM Taifa yaketi, uchaguzi wawadia