Uwanja wa Benjamin Mkapa, huenda ukaondolewa kwenye viwanja vinavyokidhi viwango kwa ajili ya kutumika kwenye Michuano ya Kimataifa ngazi ya Vilabu (Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika).

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapioshwa na Gazeti na Mwanaspoti imeelezwa kuwa, Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limeshauri Uwanja wa Benjamini Mkapa kutotumika kwa kile kilichoelezwa umeharibika eneo la kuchezea (pitch), na sasa utafungwa kwa mwezi mmoja kupisha marekebisho.

Hivyo basi, baada ya mchezo wa Jumatano ya Ligi Kuu kati ya Young Africans na KMC FC, itakayochezwa kuanzia saa 10:00 jioni uwanja huo utafungwa.

Kwa mujibu wa matumizi ya uwanja huo, unapaswa kutumika mara tatu kwa wiki lakini hadi leo itakuwa ni mara ya nne kinyume na matumizi ya uwanja huo ambao hata kabla ya hapo ulilalamikiwa kutokuwa katika hali nzuri hasa eneo la kuchezea (pitch), kwani matumizi yamekuwa makubwa.

Uwanja wa Benjamin Mkapa unatumiwa na Klabu ya Simba SC inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi pamoja na Young Africans inayoshiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mrembo Nadia Nakai afunguka mazito baada ya mazishi ya AKA
Historia: Biblia kongwe Duniani kuuzwa kwa mnada