Uongozi wa Klabu ya Dodoma Jiji FC kwa kushirkiana na Uongozi wa Uwanja wa Jamhuri umefanya maboresho kwenye vyumba vya kubadilishia vya Uwanja huo.

Dodoma Jiji FC ambayo huutumia Uwanja huo kama nyumbani kwake katika michezo ya nyumbani ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ imefanya maboresho hayo, ili kuendana na mapendekezo ya Bodi ya Ligi ‘TPLB’ na Shirikisho la soka nchini ‘TFF’.

Mapema leo Jumatano (Novemba 10), Picha za vyumba vya kubadilishi vya Uwanja huo zimeanikwa hadharani kupitia mitandao ya kijamii, huku vikionekana kuwa na mandhari ya kisasa.

Msimu huu 2021/22 Dodoma Jiji FC imeshautumia Uwanja wa Jamhuru katika mchezo mitatu ya Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting uliomalizika kwa wenyeji kupata ushindi wa 1-0, kisha wakaikaribisha Simba SC na kukubali kichapo cha 1-0 na baadae waliichapa Tanzania Prisons 2-1.

Shisha lageuka kuwa janga
Intanenti yarudishwa baada ya kuzimwa kwa wiki mbili