Uongozi wa Klabu Bingwa nchini England Manchester City umetenga kiasi cha Pauni Milioni 300 kwa ajili ya kuongeza viti vya mshabiki ndani ya Uwanja wa Etihad, kwa mujibu wa ripoti.

Mpango wa klabu hiyo ni kuongeza viti 7,700 vya mashabiki na kufikia mashabiki 61,000 ambao wataingia katika Uwanja wa Etihad na kuangalia Michezo ya Ligi Kuu na ile ya Kimataifa.

Lakini mchakato huo utajumuisha pia ujenzi wa hoteli, sehemu ya kupumzikia mashabiki na jengo la makumbusho karibu kabisa na Uwanja wa Etihad.

Jumla ya matumizi katika mchatako huo imetajwa kuwa Pauni Bilioni 1 ikiwa ni pamoja na kuboresha Uwanja wa Etihad, uwanja wa mazoezi na vituo vya kijamii yakiwamo maduka.

Makubaliano kati ya mashabiki na wakazi wa eneo hilo kuhusu mradi huo yalimalizika mwishoni mwa juma lililopita, na hatua inayofuata ni Klabu ya Man City kupewa ruhusa ili mchakato huo uanze haraka iwezekanavyo.

Endapo Man City itakubaliwa, ujenzi utaanza Novemba mwaka huu na matarajio ni kumaliza ujenzi kuanzia msimu wa 2025 na 2026.

Man City inataka ujenzi wa mradi huo upangwe kwa kuzingatia ratiba isiingiliane na msimu ili kuepuka usumbufu wowote utakaojitokeza. Kampuni ya Populous iliyoandaa mchoro wa ukarabati huo ndiyo iliyofanya kazi ya kibabe kabisa ya Uwanja wa Tottenham na wa Lyon.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo April 1, 2023
Mradi ufugaji Jongoo Bahari kuwaneemesha Wananchi