Uongozi wa klabu ya Man Utd, umedhamiria kuongoza jukwaa katika sehemu ya uwanja wa Old Trafford, ili kuuwezesha kuchukua zaidi ya mashabiki mashabiki 80,000 walioketi.

Kwa sasa uwanja wa Old Trafford una uwezo wa kuchukua mashabiki 75,635 walioketi, hivyo jukwaa litakaloongezwa litakua na viti vya mashabiki 7500.

Miongoni mwa viti hivyo vitakavyoongeza, tayari imefahamika, viti 3000 vitatengwa kwa ajili ya mashabiki wenye ulemavu ambao wamekua wakiongezeka siku hadi siku, kwa ajili ya kushuhudia michezo inayochezwa uwanjani hapo.

Hata hivyo taarifa zilizotolewa na kituo cha televisheni cha ESPN, zimeeleza kwamba, jukwaa litakaloongezwa uwanjani hapo, litapewa jina la mkongwe wa klabu hiyo Sir Bobby Charlton na kuitwa Sir Bobby Charlton stand.

Sir Bobby Charlton will have a the main stand named after himMkongwe wa klabu ya Man Utd  Sir Bobby Charlton

Kwa sasa uwanja wa Old Trafford una majukwaa manne tofauti ambayo yanajulikama kwa majina ya Sir Alex Ferguson Stand, South Stand, West Stand na East Stand.

Kazi hiyo ya kuongeza jukwaa itafanywa, ikiwa ni miaka kumi imepita, baada ya kuongezwa kwa viti 7,000 mwaka 2006.

Endapo mipango itakwenda kama inavyopangwa hivi sasa na viongozi wa Man Utd, klabu hiyo itaendelea kuwa na uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki wengi barani Ulaya, ukitanguliwa na klabu ya FC Barcelona yenye uwanja wa Camp Nou wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 99,354.

Kwa nchini England Man Utd wataendelea kuwa na uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki wengi zaidi ukifuatiwa na uwanja wa Arsenal (Emirates Stadium) wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,260 na nafasi ya tatu ikishikwa na Man city wenye uwanja wa Etihad ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 55,097.

Mayanja: Isihaka Amebadilika Kitabia
Jerry Muro Alia Na Mlolongo Wa Michezo Inayowakabili