Shirikisho la soka duniani FIFA limeitaka kamati ya maandalizi ya fainali za kombe la dunia iliyo chini ya serikali ya nchini Urusi, kukamilisha kwa wakati ujenzi wa uwanja wa Samara (Cosmos Arena) ambao ni mmoja wa viwanja vitakavyotumika katika fainali hizo.

FIFA wameitaka kamati hiyo kufanya hivyo, baada ya kufanya ukaguzi katika viwanja vyote vitakavyotumika katika fainali za mwaka huu, na kubaini bado kuna matengenezo yanaendelea kwenye uwanja huo.

Uwanja wa Samara unaochukua mashabiki 45,000 walioketi, kwa sasa unaendelea kufanyiwa matengenezo katika neo la kuchezea na kamati imeombwa kuhakikisha hatua hiyo inakamilishwa ndani ya miezi mitatu iliyosalia kabla ya kuanza michuano mnamo Juni 14.

Uwanja huo unatarajia kuwa mwenyeji wa mchezo wa kundi E, ambapo Costa Rica watapapatuana na Serbia, Juni 17.

Urusi imeandaa viwanja 12 ambavyo vitatumika kwa ajili ya michezo ya fainali za kombe la dunia za mwaka huu ambavyo ni  Luzhniki Stadium Otkritie Arena (Spartak Stadium), Krestovsky Stadium (Saint Petersburg Stadium), Kaliningrad Stadium, Kazan Arena, Nizhny Novgorod Stadium, Cosmos Arena, Volgograd Arena, Mordovia Arena, Rostov Arena, Fisht Olympic Stadium (Fisht Stadium) na Central Stadium (Ekaterinburg Arena).

Kesi ya Nondo yasogezwa mbele, akana mashtaka yanayomkabili
Mario Balotelli huenda akarejeshwa kikosini