Mpambano wa ligi kuu ya soka Tanzania bara utakaowakutanisha vinara wa msimamo waligi hiyo Wekundu wa Msimbazi Simba dhidi ya mabingwa watetezi Young Africans Jumapili Aprili 29,2018, umepangwa kuchezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa na tiketi zinaendelea kuuzwa kupitia Selcom.

Shirikisho la soka nchini TFF limewataka mashabiki wa soka waliopanga kuushuhudia mchezo huo wakiwa uwanjani, kununua tiketi zao kupitia Selcom, kwa kufuata utaratibu wa kieletroniki.

TFF imewaomba mashabiki kuhakikisha wanajaza kujaza pesa kwenye kadi zao za Selcom ambazo zitawawezesha kununua tiketi hizo, kupitia simu ya mkononi.

Katika hatua nyingine TFF, imethibitisha taarifa za kufunguliwa kwa mageti ya uwanja wa taifa kufunguliwa mapema kuanzia saa 2 asubuhi ambapo vyakula na vinywaji vitapatikana ndani.

Kwa upande wa ulinzi na usalama wa mashabiki, Jeshi la Polisi limehakikisha ulinzi utakua wa hali ya juu na kuwatahadharisha wale wote wenye nia ya kufanya vitendo vya uovu.

Mamlaka ya Uwanja imethibitisha kuongezeka kwa camera za Uwanjani ambapo sasa zimefikia 109 ambazo zitakuwa zinafuatilia matukio yote.

Video: Majaliwa aridhishwa na maandalizi sherehe za miaka 54 ya Muungano
Ngorongoro Heroes wapewa mapumziko