Mamlaka ya majisafi Tanga (Uwasa) imetangaza mkakati wa kuingia kwenye teknolojia ya ufungaji wa mita za maji zitakazo kuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe na kutuma taarifa makao makuu ya mamlaka hiyo.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Ankara wa Uwasa, Daudi Mkumbo juzi wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Duga kuhusu huduma  za maji.

Amesema mita hizo zitakuwa zimefungwa chombo kitakachokuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe na watu ambao wanashughulika na usomaji wa mita watakwenda kufanya kazi nyingine hali itakayorahisisha usomaji wake.

“Tunaamini uwepo wa mita hizo utaondoa changamoto kwa baadhi ya wateja wanao dai kwamba wasomaji hawafiki kwenye maeneo yao kusoma mita” ameeleza Mkumbo.

Kwa upande wa wananchi wamesema kuwa wanatarajia njia hiyo itawasaidia kuepuka hasara waliyokuwa wanaipata awali kwani walikuwa wanalipa ankara kubwa hata kipindi ambacho maji huwa yanakatika.

Haiti wafanya kumbukumbu miaka 10 ya Tetemeko baya
Taiwan wamchagua Rais Mwanamke kuwaongoza muhula wa pili ”Vita dhidi ya China”