Ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara baina ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki – EAC, vikwazo vingine vipya vinne vimewasilishwa, huku zikikubaliana kuondoa vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha – NTBs na vikwazo nane vikiendelea kushughulikiwa.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki – SCTIFI, uliofanyika Juni 3, 2023 Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha.

Wakizungumza baada ya Mkutano huo, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wamesema Baraza hilo la Mawaziri wa Kisekta, pia limekubaliana kutoza dola 10 za kimarekani kwa kilomita 100.

Tozo hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya barabara kwa malori ya mizigo yanayofanya safari katika nchi wanachama badala ya kila nchi kutoza gharama zake, na kuimarisha utoaji huduma za forodha katika mpaka wa Kenya na Tanzania, ili kupunguza msongamano wa malori.

Aidha, Baraza hilo la Mawaziri la Kisekta, limekubaliana kuondoa gharama ya viza kwa watu wanaotaka kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kibiashara, ili kukuza mahusiano miongoni mwa wakazi wa Jumuiya hiyo pamoja na kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi wa nchi husika.

Kuhusu uondoshaji wa mizigo, Mawaziri hao walifahamishwa kuwa mizigo ya Tanzania inayosafirishwa kwenda Kenya itaendelea kuondoshwa kupitia Mfumo wa Himaya Moja ya Forodha ulioanza kutumika kuanzia mwezi Aprili 2023.

Mkutano huo, pia umeidhinisha Rasimu ya Mwisho ya Viwango vya Afrika Mashariki (FDEAS) ambapo viwango 65 vitaanza kutumika rasmi, umepitisha Andiko la Kisera kwa ajili ya EAC kufanya majadiliano na maeneo mengine ya Kikanda na nchi nyingine, Hadidu za Rejea.

EAC pia zimekubaliana kutoza kiwango cha dola 10 za kimarekani kwa kilomita 100 kwa ajili ya matumizi ya barabara (road user charge) kwa magari ya mizigo kutoka nchi moja kwenda nyingine katika Jumuiya hiyo badala ya kila nchi kuwa na viwango vyake vya tozo.

Kipa Young Africans atoa kauli ya kishujaa
Dante awachimba mkwara askari magereza