Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema zoezi la uzimaji moto katika Mlima Kilimanjaro linaendelea vyema licha ya changamoto mbalimbali za upepo unaozidisha kasi ya moto, maporomoko ya mawe na uoto wa asili ambao umekuwa ukisababisha kuchelewa kwa ufanisi wa zoezi hilo.

Majaliwa ameyasema hayo hii leo Novemba 3, 2022 Bungeni jijini Dodoma wakati akitoa taarifa fupi na kuongeza kuwa athari ambazo zingeweza kuletwa na moto huo zimedhibitiwa kwa sehemu na kwamba kwa ushirikiano na Jeshi wameweza kuendelea kuuzima moto huo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Amesema, ” Zoezi la uzimaji moto katika Mlima Kilimanjaro linaendelea vizuri licha ya changamoto mbalimbali kama upepo ambao umekuwa ukivuma na kuongeza kasi ya moto lakini pia kuna uoto wa asili ambao umekuwa ukisababisha kuchelewa kwa ufanisi wa zoezi hilo.”

Mapema mara baada ya kuanza kwa moto huo hivi karibuni, Wanasayansi walionya kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu yanaendelea kusababisha athari ikiwemo hali mbaya ya hewa, kuongezeka kwa joto duniani na ukame.

Simba SC yazitaka 18 za Novemba
Nassib Ramadhan atamba kumchakaza Helebe