Uzinduzi wa taasisi  ya maridhiano Tanzania imeundwa na viongozi wa madhehebu mbalimbali nchini ili kuleta  umoja,amani,na maridhiano katika jamii  na inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 13/7/2016,katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam namgeni rasimi  anatarajiwa kuwa ni Waziri wa mambo ya ndani Mh.Mwigulu Lameck Nchemba,

Hayo yamesemwa na Sheikh Sadick Godigodi kwa kushirikiana na Mchungaji Oswald Mlay mapema hii leo , chama hicho kitakuwa kinashirikiana kwa karibu na serikali  na kukutanisha madhehebu  yote ya dini nchini  kwa lengo la kutoa elimu,kulinda na kudumisha amani ya nchi hivyo kutoa utatuzi katika masula yote yanayoleta changamoto kwa jamii.

Aidha mchungaji Mlay aliongeza kuwa chama hicho kinategemea  kuwa msuluhishi mkubwa wa migogoro chochezi  ya kidini na  kutoa elimu kwa umma, wafugaji na wakulima,kushirikiana katika mipango mikakati yenye kushughulikia majanga ya madawa ya kulevya  kwa jamii ya kitanzani.

Naye Sheikh Godi godi alisema katika uzinduzi huo kutakuwa na shughuli mbalimbali za utoaji tuzo za amani ili kuthaminisha  vitendo vya makusudi katika jamii yenye kulinda,kujenga na kuiboresha jamii ili kuwepo uthibitisho wa ujenzi wa amani.

Lengo kuu la tuzo hizo za amani za kila mwaka  ni pamoja na  kujenga juhudi endelevu za wananchi kuishi kwa amani,kuheshimiana nakuvumiliana katika tofauti za kiitikadi za kidini au imani za aina yeyote ile katika nchi na kauli mbiu ni ‘’Tanzania ni Yetu Amani Kwanza’’

Watu wanaotarajia kupata tuzo ni pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete,Mwanzilishi na spika wa Bunge la Uchumi Tanzania Albert Sanga,Mama Maria Nyerere,IGP mstaafu,Mrs Helen Kijo-Bisimba na wanaharakati mbalimbali.

CAF Wasikia Kilio Cha Young Africans
Mr Blue aeleza alivyokacha uvutaji bangi, ulevi na kufanikiwa