Makamu wa Rais AS Monaco Vadim Vasilyev amezisemea mbovu klabu za Man Utd na Chelsea zote za nchini England kufuatia kushindwa kumtumia ipasavyo mshambuliaji kutoka nchini Colombia Radamel Falcao.

Falcao alifunga mabao matano kwa kipindi cha miaka miwili aliyocheza soka nchini England kwa mkopo akiwa na klabu hizo, lakini kwa sasa anaonyesha kurejea katika hali yake, tangu alipojiunga tena na AS Monaco.

Vasilyev amehojiwa na gazeti la Daily Mail na kutoa lawama kwa viongozi wa mabenchi ya ufundi ya klabu za Chelsea na Man Utd kwa kusema walishindwa kumpa muda mshambuliaji huyo ili afanikishe azma ya kucheza soka la ushindani na kufunga mabao.

“Sifahamu kwa nini Man Utd na Chelsea walishindwa kuwa wavumilivu katika hatua za kumtumia Falcao katika kipindi cha msimu mmoja kwa kila klabu aliyoicheza kwa mkopo.

“Katika soka unapaswa kuwa mvumilivu, daima mchezaji hawezi kuwa katika hali yake ya kawaida, hasa anapotoka katika matatizo ya kujiuuguza, jambo hilo AS Monaco tumelifahamu na ndio maana kwa sasa anacheza soka lake vizuri.

“Kama itatokea unamsajili mchezaji kwa maslahi ya kukusaidia wakati wote bila kujali katika soka kuna wakati mambo huwa magumu, lazima mpango wako utashindwa kufanya kazi kwa namna ambavyo unafikiria, hivyo ndivyo ilivyokua kwa Man Utd na Chelsea, walimtarajia Falcao kwa makubwa zaidi wakati walitambua alikua anatoka katika kipindi kigumu cha kujiuguza geraha la mguu.”

“Falcao alihitaji muda na kupewa nafasi kadri inavyowezekana ili aonyeshe uwezo wake, lakini katika ligi ya England ilikua tofauti na alivyorejea Ufaransa ambapo kwa sasa anaonyesha uwezo wa kucheza soka lake la ushindani na kila mmoja ameanza kufurahi.

“Amekua Falcao ambaye tulimzoea, na bado ninaamini mambo mengi mazuri yanakuja kutoka kwake.

“Kwa sasa anafunga mabao, na amekua muhimili mkubwa kikosini na wakati mwingine huwahimiza wachezaji wenzake wa AS Mocano ili wajitume kwa manufaa ya kusaka ushindi. Amesema Vadim Vasilyev

Marekani yaweka vitisho Korea Kusini, Ndege za kivita zapaa angani
Ryan Babel Abisha Hodi Amsterdam Arena