Klabu ya Man Utd imethibitisha, itamuachia mlinda mlango Victor Valdes itakapofika mwezi januari mwaka 2016, wakati wa dirisha dogo la usajili litakapo funguliwa.

Valdes, mwenye umri wa miaka 33, amekua na mazingira magumu ndani ya klabu hiyo yenye historia kubwa nchini England pamoja na barani Ulaya, kufuatia kushindwa kutimiza malengo ya kucheza mara kwa mara, kwani mpaka sasa ameshajumuishwa kikosini mara mbili tangu aliposajiliwa miezi kumi iliyopita.

Kuruhusiwa kuondoka klabuni hapo itakapofika mwezi januari, pia kunasukumwa na mahusiano mabaya yaliyojengeka baina ya mlinda mlango huyo ambaye aliwahi kuwika akiwa na klabu ya Barcelona dhidi ya meneja wa Man Utd, Louis van Gaal.

Tayari Valdes, ameshaanza kuhusishwa na mipango ya kutaka kuhamia kwenye klabu ya Newcastle Utd, ambayo imeanza kumsaka mbadala wa mlinda mlango wao mashuhuri, Tim Krul aliye majeruhi kwa sasa.

Valdes, ana histoatia yake nchini kwao Hispania, baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2010, pamoja na kile kilichotawazwa kuwa mabingwa wa barani Ulaya mwaka 2012.

Kwa upande wa klabu ya FC Barcelona, Valdes alifanikiwa kuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa La Liga mara sita, ligi ya mabingwa barani Ulaya mara tatu pamoja na Spanish Cup mara mbili.

Boban: Mbeya City ‘Itaiadhibu’ Simba Jumamosi
Lowassa: Hakuna Wa Kutuzuia…