Beki kutoka nchini Colombia Jeison Murillo amekamilisha safari ya kujiunga na Valencia CF ya nchini Hispania kwa mkopo, akitokea mjini Milan Italia kwenye klabu ya Inter Milan.

Valencia CF wamekamilisha mpango huo, na kumsainisha Murillo mkataba wa miaka miwili ambao utafikia kikomo mwishoni mwa msimu wa 2018/19.

Hata hivyo katika makubaliano ya klabu hizo, kuna uwezekano wa beki huyo mwenye umri wa miaka 25 akasajiliwa moja kwa moja huko Estadio Mestella, endapo ataonyesha kiwango kitakachoridha katika kipindi chote cha miaka miwili.

Murillo anaungana na beki wa kibrazil Gabriel Paulista aliyesajiliwa na Valencia katika kipindi hiki akitokea kwa washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal).

Andrea Barzagli: Juvuntus Hatutoyumba
Kamati Ya Katiba, Sheria Na Hadhi Za Wachezaji Kuamua Utata Wa Usajili