Klabu ya Valencia ya nchini Hispania imejinasibu kuwa tayari kupokea ofa kutoka kwenye klabu yoyote, ambayo ipo tayari kumsajili beki kutoka nchini Ujerumani, Shkodran Mustafi.

Taarifa hizo kutoka Estadio Mestalla, huenda zikawa faraja kwa meneja wa klabu ya Arsenal (Arsene Wenger), ambaye ameonyesha nia ya kumsajili Mustafi, baada ya kuumiwa kwa beki wake kutoka nchini Ujerumani Per Mertesacker ambaye atakosa baadhi ya michezo ya ligi kuu ya England itakayoanza mwezi ujao.

Ada ya usajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24, imetajwa kuwa Euro milioni 50, lakini Wenger ameonyesha kuwa tayari kumsajili Mustafi kwa Euro milioni 25.

Mustafi ameshawahi kucheza soka nchini England akiwa na kikosi cha vijana cha Everton mwaka 2009, baada ya kusajiliwa akitokea kwenye klabu ya Hamburger SVya nchini kwao Ujerumani.

TBL Yaiweka Njiapanda Simba SC
Antonio Conte: Soko La Usajili Limekua Na Changamoto Kubwa