Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa, Valere Germain amekamilisha dili la kujiunga na klabu ya Olympic Marseille akitokea kwa mabingwa wa Ligue 1, AS Monaco.

Germain mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Olympic Marseille kwa mkataba wa miaka minne, baada ya kufaulu vipimo vyake ya afya. Lakini ada yake ya uhamisho imefanywa kuwa siri.

Msimu uliopita Germain aliifungia AS Monaco mabao 10 na kuiwezesha timu hiyo ya Stade Louis II kutwaa ubingwa wa kwanza wa Ligue 1 tangu mwaka 2000.

Germain anakuwa mchezaji wa pili kuihama AS Monaco katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi. Akitanguliwa na Mreno Bernardo Silva aliyejiunga na Manchester City kwa ada ya Pauni milioni 43.

Paolo Maldini Atupwa Nje Aspria Tennis Cup
Ujerumani yaitupa nje Uingereza michuano ya U21