Meneja wa Manchester United Louis van Gaal, amesema haoni haja ya kujiuzulu baada ya timu yake kutoka sare ya 0-0 na Chelsea uwanjani Old Trafford.

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika Van Gaal alisema “kama wachezaji wanaweza kucheza kwa kiwango kile wakiwa kwenye shinikizo hakuna sababu ya kujizulu”.

Kocha huyo amekua kwenye shinikizo kubwa la kumtaka kujiuzulu kufuatia kikosi hicho kuchapwa michezo minne mfululizo kipigo cha mwisho kikiwa kutoka kwa Stoke City Jumamosi walipocharazwa 2-0.

Man United wameshindwa kupata ushindi katika michezo minane ya mashindano yote waliyoshiriki msimu huu. Hii ni mara ya kwanza klabu hiyo kufanya hivyo tangu mwaka 1990.

Klabu hiyo kwa sasa imo nambari sita kwenye jedwali na alama tano nyuma ya klabu iliyo nambari nne ligini.

“Katika ulimwengu huu wazimu wa soka, hili linaweza kufanyika siku yoyote ile na kwangu pia,” alisema. “Ukizingatia kwamba ilimfanyikia Jose Mourinho, basi inaweza kunitendekea.

Mourinho alifutwa kazi na Chelsea baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya, licha yake kuwaongoza kushinda taji la ligi msimu uliopita.

Meneja huyo ni mmoja wa wanaodhaniwa wanaweza kumrithi Van Gaal iwapo ataondoka Old Trafford na wakati wa mechi hiyo dhidi ya Chelsea, kuna mashabiki waliovalia mavazi yenye jina lake.

Yanga Uso Kwa Macho Na Azam FC Mapinduzi CUP
Slavisa Jokanovic Meneja Mpya Craven Cottage