Bosi wa kikosi cha Man Utd, Louis van Gaal ameonyesha kukabiliwa na mtihani mzito wa kufikia malengo yaliyowekwa na viongozi wa klabu hiyo, ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa michuano wanayoshiriki tangu alipokubali kusaini mkataba wa kuitumikia The Red Devils mwaka 2014.

Van Gaal, ameonyesha kukabiliwa na mtihani mzito, baada ya kukiri huenda ikawa ngumu kwake kukiwezesha kikosi cha Man Utd kutwaa ubingwa, kutokana na ratiba ya ligi ya nchini England kumbana kiswa sawa.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, kuelekea katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili, ambapo mashetani wekundu watawakaribisha Man city kwenye uwanja wa Old Trafford, meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, amesema ni vigumu kwa yoyote kufikia lengo kutokana na ratiba kubana.

Amesema kikosi chake kinaelekea katika mpambano huo wa jumapili, ikiwa ni siku tatu baada ya kutoka nchini Urusi walipokwenda kucheza mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya CSKA Moscow, na kuambulia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Van Gaal ameongeza kuwa safari, yao ilikuwa na umbali wa maili 3,200, hali ambayo dhahiri imewachosha wachezaji wake ambao walihitaji kupumzika kwa zaidi ya siku tatu kabla ya kupambana na wapinzani wao wa mjini Manchester.

Jambo lingine ambalo Van Gaal anaamini ni kikwazo kwa kikosi chake kufikia malengo, ni kushindwa kupatikana kwa muda wa ligi ya nchini England kusimamishwa kama ilivyo kwenye ligi nyingine barani Ulaya, ambapo inapofika mwishoni mwa mwaka hupigwa kalenda hadi mwanzoni mwa mwaka unaofuata.

Amekiri ligi ya England ni ngumu kutokana na kila timu kuwa katika hali ya ushindani, hivyo unapomtumikisha mchezaji kwa muda wa miezi minane mfululizo kwenye michuano tofauti ni dhahir atachoka na wakati mwingine kukatishwa tamaa na matokeo kama hayatokua mazuri.

Kutokana na malalamiko hayo, Van Gaal amekitaka chama cha soka nchini England kufikiria upya namna ya kuzisaidia klabu za England, ili ziweze kupata muda wa kuwapumzisha wachezaji wake, na wakati mwingine kutoa mwanya wa kuitazama hata timu yao ya taifa, ambayo bado inawahitaji wachezaji hao hao.

Hatimaye Mahakama Yatoa Hukumu Kesi Ya 'Mita 200', Iko Hapa
Magufuli Amvaa Lowassa Dakika Za Mwisho, Atahadharisha