Baadhi ya vyombo vya habari nchini Ujerumani, vimefichua siri iliyokua imejificha miongoni mwa viongozi wa klabu ya Man Utd pamoja na FC Bayern Munich iliyokuwa inamhusu mshambuliaji Thomas Muller.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimelazimika kufichua siri hiyo baada ya kubaini kulikuwa na mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo viongozi wa Man Utd walionyesha dhamira ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 100.

Imebainika kwamba mazungumzo baina ya pande hizo yaliishia gizani, kufuatia uongozi wa klabu ya Bayern Munich, kuweka msimamo wa kutomuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kwa kuamini bado huduma yake inahitajika huko Allianz Arena.

Meneja wa klabu ya Man Utd, Louis van Gaal anatajwa kuwa chanzo kikubwa cha kutoa msukumo kwa mabosi wake huko Old Trafford kukamilisha mpango huo kutokana na kuamini uwezo wa Muller ungekisaidia kikosi chake kufikia lengo la kurejesha heshima humo nchini England pamoja na barani Ulaya.

Van Gaal aliwahi kufanya kazi na Muller wakati akiwa meneja wa FC Bayern Munich kuanzia mwaka 2009–2011.

Tayari meneja huyo kutoka nchini Uholanzi ameshafanikiwa kumsajili kiungo Bastian Schweinsteiger, akitokea FC Bayern Munich, kwa lengo la kukamilisha sera yake ya kuwapata wachezaji ambao waliwahi kufanya nao kazi kwa mafanikio makubwa.

Chadema Yamfungulia Mlango Lowassa Kiroho Safi, Dr. Slaa Azungumza
Fupa La Kibrazil Lamshinda Mourinho, Kulirudisha Alikolitoa