BOSI wa Mashetani Wekundu, Louis Van Gaal amesikiliza tetesi na tarifa zinazoihusisha AC Milan kutaka kumchukua kwa mkopo Marouane Fellaini.

Tarifa za motomoto kutoka katika viunga vya Old Trafford zimebainisha kuwa ombi la klabu hiyo ya San siro, ni kama vile limemegonga mwamba baada ya Van Gaal kusema “no” haiwezekani. Kasha bosi huyo raia wa Uholanzi akaipasha AC Milan kuwa bado kiungo huyo ana nafasi ndani ya United na kwamba hawezi kuondoka katika mazingira yoyote ya kwenda kucheza kwa mkopo katika klabu yoyote.

Fellaini alitua Old Trafford kwa kitita cha pauni mil 27.5 akitokea Everton mnamo mwezi Agosti, 2013, lakini anajikuta hana msimu mzuri chini ya Van Gaal.

Van Gaal amempanga kiungo huyo katika michezo mine ya Ligi ya Premier, ambapo kwa sasa yuko katika kampeni ya kuendelea kumshawishi Mholanzi huyo ili kuweza kupata namba ya kudumu kikosini. Lakini taarifa kutoka nchini Italia zinathibitisha kuwa, AC Milan wamepiga hodi Old Trafford na kuleta ombi la kumsainisha kwa mkopo raia huyo wa Ubelgiji, hususan katika kipindi hiki cha kufunguliwa kwa dirisha la usajili la mwezi Januari.

Hatua ya AC Milan kumwitaji Fellaini inakuja wakati ambapo Manchester United imo katika wimbi la lawama kutoka kwa wadau na mashabiki wa klabu hiyo wanaolalamikia kuondoka kwa baadhi ya wanandinga ambao kwa sasa wanafanya vyema katika timu zao za sasa ilihali United ikikabiliwa na mwendo wa kusuasua.

Wachezaji hao ni pamoja na Robin Van Persie, Radamel Falcao na Javier Hernandez ambapo tayari kocha Van Gaal amesikika akinukuliwa kuwa hakufanya uamuzi wa busara kuwaruhusu waondoke Old Trafford.

Wabunge wacharukia Bomoabomoa
Claudio Ranieri Akiri Kuwa Na Kibarua Kigumu Bila Jamie Vardy