Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba SC Sven Ludwig Vandenbroeck amesema hana mpango wa kumsajili mchezaji yoyote wa klabu hiyo ya Dar es salaam.

Sven ambaye aliondoka Simba SC mwishoni mwa mwaka 2020, ameweka wazi msimamo wake huo, Kufuatia nchi nyingi duniani kuwa kwenye msimu wa usajili.

Kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji amesema licha ya klabu yake ya zamani (Simba SC) kuwa na wachezaji wazuri na wenye ubora mkubwa, lakini hafikirii kuwasajili kwa sababu tayari wachezaji hao wana mikataba.

Amesema ili awasajili wachezaji hao hana budi kulipa kiasi cha pesa kisichopungua $1m (dola milioni moja) kama fidia za kuvunja mikataba yao.

“Licha ya Simba kuwa na wachezaji wazuri sana lakini sifikirii kusajili mchezaji yeyote kutoka katika klabu hiyo kwasababu tayari klabu ya Simba imewasainisha mikataba mirefu.”

“Hivyo ili kuwapata itakubidi uwalipe ada ya usajili kiasi cha pesa kisichopungua dola milioni moja” amesema Sven

Sven anakinoa kikosj cha ASFAR ya Morocco, na msimu uliopita ameiwezesha timu hiyo kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye ligi ya Morocco.

Duchu kuondoka Simba SC
Manara: Sitokuwepo Kigoma, nitasali ili tushinde