Vanessa Mdee amerusha ‘jiwe zito gizani’ kupitia mitandao ya kijamii akimlenga mwanaume mwenye tabia za usaliti na uongo.

Ujumbe wa mwimbaji huyo wa ‘Moyo’ umewafanya baadhi ya watu kudhani kuwa jiwe hilo lilikuwa limeelekezwa kwa aliyekuwa mpenzi wake, Juma Jux.

“A good woman will stay by your side no matter how much you lie, cheat or steal. That woman is your mother not us,” ameandika Vanessa.

Kwa tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi ujumbe huo, “mwanamke mwema atakuwa na wewe bila kujali ni mara ngapi umemdanganya, umemsaliti au umeiba. Huyo mwanamke ni mama yako mzazi sio sisi.”

Maandishi hayo ya Vee Money yamesababisha baadhi ya watu kuamini kuwa aliyoyataja hapa ndiyo yaliyomfanya ashindwe kubaki pembeni ya Jux kwakuwa anaamini hakuna mwanamke anayeweza kuyavumilia isipokuwa mama mzazi ambaye hamuachi mwanaye.

Tetesi za uhusiano wa mapenzi kati ya wasanii hao zilianza mwishoni mwa mwaka 2012, ingawa waliweka wazi uhusiano wao kati ya mwaka 2014 na 2015.

Mwaka juzi, penzi lao lilipata mtikisiko na wakatangaza kuachana, lakini walirejesha tena uhusiano wao.

Hata hivyo, bundi ametua tena kwenye uhusiano wao na wametangaza kuachana tena huku Vanessa akidai ‘wamebaki kuwa marafiki’.

Hivi karibuni Jux aliachia wimbo uitwao ‘Sumaku’ aliomshirikisha Vanessa na wote walionekana kuupigia debe kwa mashabiki.

Waziri ataka sheria ya matusi isitungwe, adai matusi huongeza afya
Kuna watu wanaropoka tu huko- Uhuru Kenyatta

Comments

comments