Mwimbaji Vanessa Mdee anazidi kuimarisha ngome ya muziki mzuri na kuongeza idadi ya mashabiki kwa kumvuta mkali wa RnB na Bongo Fleva, Maua Sama kutikisa anga la Bongo Fleva.

Vee Money ambaye anatamba na wimbo wake ‘Kisela’ aliomshirikisha Mr P wa P Square kutoka Nigeria amesema kuwa tayari wameshapika wimbo wao na kwamba hivi karibuni watauachia.

“Wimbo tumeufanya katika studio za ‘B Catch’ na mtayarishaji mmoja anaitwa Breezy,” alisema Vanessa ingawa hakuweka wazi jina la wimbo husika.

Muunganiko wa Vanessa na Maua Sama ambaye anafanya vizuri na wimbo wake ‘KatuKatu’ una kila dalili za kuzaa kitu kikubwa kwa ajili ya mashabiki, na huenda Vanessa akawa amemshika mkono Maua kumpandisha kwenye jukwaa la kimataifa kama alivyo yeye.

Hii ni collabo ya kwanza kufanywa na wasanii hao wa kike na kuongeza idadi ya collabo za wasanii wa kike ambazo ni adimu au chache kusikika kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Video: Lissu aizulia jambo Bombardier, Ugonjwa wa Manji selo waahirisha kesi yake
Young Dee aitetea ‘Bongo Bahati Mbaya’ dhidi ya tuhuma...