Aliyekuwa wanamuziki mahiri wa Bongo fleva Vanessa Mdee, ametoa wito kwa wasanii na watu mashuhuri nchini kuepuka kujiingiza kwenye mikataba na makampuni au taasisi mbalimbali kabla ya kujiridhisha juu uhakika wa hatma ya makubaliano yao.

Vanessa ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kubainisha kuwa yeye ni muhanga wa changamoto zilizotokana na Bank aliyoingia nayo mkataba wa kazi kukiuka matakwa ya mkataba huo.

Jambo hilo limesababisha Vanessa kubaki akiidai Bank hiyo kiasi cha pesa kwa kipindi kirefu bila mafanikio.

“Artists na watu maarufu Tanzania please don’t let these corporate companies take advantage of you. Mpaka leo lile benki halijamaliza kunilipa. Japo kiukweli ni benki bora but wameona wajikaushe. Yote kheri” ameandika Vanessa.

Vanessa ameyasema hayo wakati ambao wadau mbali mbali muziki wakiendelea kutilia mkazo swala wasanii na watu mashuhuri kujikita katika kujifunza elimu ya mikataba ili kufahamu kwa undani hatua zote muhimu zinazipaswa kufuatwa ili kuepuka changamoto za namna hiyo.

Waziri Nchemba aongoza kikao kazi cha EAC
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 30, 2021