Meneja wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone anajipanga kufanya usajili wa kushangaza kwa kumchukua mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy.

Habari kutoka katika gazeti la Mirror la nchini Uingereza zinasema Vardy mwenye umri wa miaka 31 anakadiriwa kuwa na thamani ya kiasi cha paundi milioni 16 lakini Atletico Madrid wanapanga kutoa kiasi cha paundi milioni 20 kiasi ambacho kitawashawishi Leicester kufanya biashara hiyo.

Simeone anaamini Vardy atakuwa chaguo sahihi kurithi nafasi ya Antoine Griezmann ambaye anahusishwa na kutimkia Barcelona.

Atletico Madrid watalazimika kununua mshambuliaji mwingine atakaye saidiana na Diego Costa ikizingatiwa kuwa Fernando Torres naye anahusishwa na kutaka kuondoka katika klabu hiyo.

Simeone alivutiwa na kiwango cha Jemie Vardy katika ligi ya mabigwa wa Ulaya msimu uliopita na sasa anataka mshambuliaji huyo atue katika dimba la Wanda Metropolitano.

Video: Wafanyakazi DataVision wafuturu pamoja na watoto wenye Saratani Muhimbili
Dkt. Kimei amwaga chozi hadharani