Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa msaada wa miguu ya bandia aliyokuwa ameahidi huku akisema kuwa wajibu wa Serikali ni kusaidia na kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.

Ametoa msaada huo mapema hii leo jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa msaada huo wa miguu bandia itawarahisishia kufanya shughuli zao mbalimbali za kujiingizia kipato.

“Huu ni wajibu wa Serikali kutoa huduma kwa wananchi, kupunguza makali ya maisha hivyo msaada huu ni mhimu sana katika shughuli za wananchi kama hawa wenye ulemavu,” amesema Makonda.

Aidha, amesema kuwa gharama ya kununulia miguu hiyo ni kubwa hivyo huo ni wajibu wa Serikali kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wake popote pale walipo.

Video: Benki ABC yazindua huduma mpya za uwakala
Mke wa Roma: Roma alipita na baraka zangu kwenye 'Zimbabwe'