Klabu ya Wolfsburg ya nchini Ujerumani, imetoa taarifa za kutokua tayari kumuachia kiungo Julian Draxler ambaye jana mchana alikaririwa na vyombo vya habari akisema anataka kuondoka.

Taarifa iliyotolewa mapema hii leo imeeleza kuwa, uongozi wa VfL Wolfsburg haupo tayari kufanya hivyo kutokana na mkataba uliopo dhidi ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22.

Hata hivyo taarifa hiyo imeongeza kuwa, viongozi wa VfL Wolfsburg walimuita Julian Draxler na kufanya nae mazungumzo kuhusu kauli yake inayodaiwa kunukuliwa na vyombo vya habari, na wamekubaliana kwa dhati kuheshimu mkataba uliopo klabuni hapo.

Mkataba baina ya pande hizo mbili zinazodaiwa kukutana na kufikia makubaliano unaishia mwaka 2017.

Kiungo huyo ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia miaka miwiwli iliyopita, anahusishwa na mpango wa kuwindwa na washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal), na kauli yake ya jana ilionyesha kuwafurahisha mashabiki wa klabu hiyo inayonolewa na Arsene Wenger.

Jose Mourinho: Bado Usajili Wa Mchezaji Mmoja
Man City Wafanya Kweli Kwa Kinda La Kibrazil