Beki Yanga, Vicent Bossou ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Togo ambacho kinakabiliwa na mechi mbili za kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Tunisia.

Tangu asajiliwe na Yanga mwanzoni mwa msimu huu, Bossou amekuwa akiitwa na kocha wa timu ya Taifa ya Togo, Tom Saintfiet licha ya kutocheza mechi.

Saintfiet aliwahi kuinoa klabu ya Yanga na kuipa ubingwa wa Kombe la Kagame mwaka 2012 hajamjumusha kabisa kikosi mlinzi huyo wa Yanga ambaye ameanza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga kutokana na Nadir Haroub kuwa nje kwa majeruhi kwa muda.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Man City na Spurs, Emmanuel Adebayo ametoa udhuru wa kutojiunga na kikosi cha Togo akidai si wakati muafaka kwa yeye kurejea kuichezea timu yake ya Taifa.

Adebayor ambaye kwa sasa anacheza klabu ya Crystal Palace amesema kwa sasa amejikita katika kuimarisha kiwango chake katika klabu hio aliyojiunga nayo wakati wa dirisha dogo la usajili.

” Ingekuwa jambo la heshima kuchezea taifa langu. Hata hivyo nafikiri huu sio muda muafaka kufanya hivyo. Kama mjuavyo, nimesaini katika timu mpya hivi karibuni na ninafanya kila kitu kuwa katika utimamu wa mwili na kiakili”

Togo inayoongoza kundi A baada ya kushinda mechi zake mbili dhidi ya Liberia na Djibouti na kujikusanyia pointi sita itawavaa Tunisia tarehe 25 Machi jijini Lome kabla ya kurudiana nao siku nne baadaye nchini Tunisia.

Kikosi cha Togo:

Agassa Kossi (Reims, Ufaransa), Cédric Mensah (SR Colmar, Ufaransa), Abdul Gafar Mamah (Dacia Chisenau, Moldova), Serge Akakpo (Trabzonspor, Uturuki), Amevor K. Mawouna (Notts County, Uingereza)

Djene Dakonam (Alcorcon, Hispania), Kokou Donou (Enugu Rangers, Nigeria), Kossivi Nouwoklo (Togo), Sadat Ouro-Akoriko (Al Faisaly Saudi Arabia)

Joseph Douhadji (UTD Rivers, Nigeria), Kodjo Fo-doh Laba (US Bitam, Gabon), Wome Dové (Supersports United, Afrika Kusini), Akoete Eninful (Doxa Katakopias, Cyprus), Atakora Lalawele (Helsingborg, Sweden)

Mathieu Dossevi (Standard Liege, Ubelgiji), Serge Gakpé (Atalanta, Italia), Prince Segbefia (Elazigspor, Uturuki), Abraw Camaldine (Kaiser Chiefs, Afrika Kusini), Emmanuel Adebayor (Crystal Palace, Uingereza)

Foovi Aguidi (Hearts of Oak, Ghana), Alaixys Romao (Marseille, Ufaransa), Floyd Ayité (Bastia, Ufaransa), Jonathan Ayité (Alanyaspor, Uturuki), Farid Zato (Sigma Olomouc, Czech ), Peniel Mlapa (Bochum, Ujerumani)

Kuibuka Kwa Rashford Na Mkasa Wa Edibily Lunyamila
Simba Katika Mipango Ya Kurejea Kwenye Kilele Cha VPL