Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque ametaja kikosi chake cha mwisho ambacho kitakwenda nchini Ufaransa kutetea taji la barani Ulaya kuanzia Juni 10 mwaka huu.

Del Bosque, amemjumuisha beki wa kuli wa Arsenal, Hector Bellerin kama mbadala wa Dani Carvajal ambaye anasumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja, aliyoyapata wakati wa mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid.

Bellerin, mwenye umri wa miaka 21, alionekana kumshawishi kocha mkuu wa Hispania kuwa mbadala sahihi wa Carvajal, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Bosnia-Herzegovina uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Katika hatua nyingine Del Bosque, atalazimika mewaongeza wachezaji wanne katika kikosi chake cha mwisho wakitokea kwenye klabu za Atletico Madrid pamoja na Real Madrid.

Miongoni mwa walioitwa ni nahodha na beki wa Real Madrid Sergio Ramos,  Lucas Vasquez pamoja na beki wa kulia wa Atletico Madrid Juanfran sambamba na kiungo Koke.

Marco Reus Kuzikosa Fainali Za Euro 2016
Wapinzani wasusia Bunge, wapanga haya dhidi ya Naibu Spika