Kocha Vicente Del Bosque ametangaza kujizulu nafasi ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Hispania, baada ya kushindwa kufikia lengo la kutetea ubingwa wa barani Ulaya katika fainali za Euro 2016, zinazoendelea nchini Ufaransa.

Hispania ilivuliwa ubingwa katika hatua ya 16 Bora ya michuano ya Euro baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Italia.

Del Bosque ameamua hivyo na taarifa zikafikishwa kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Hispania, Angel Villar.

Imeelezwa, awali Del Bosque alizungumza na rais huyo siku ya Jumanne, lakini kiongozi huyo wa soka nchini Hispania, ilionekana kama hakukubaliana na uamuzi wake. Huenda kulikuwa na namna ya kutaka kumshawishi abaki.

Kocha huyo aliiwezesha Hispania kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2010 na kisha ubingwa wa barani Ulaya katika fainali za Euro 2012.

Pia inaelezwa, De Bosque alimueleza rais huyo kwamba hata kama angechukua ubingwa Euro 2016, hakuwa na mpango wa kuendelea baada ya fainali hizo kumalizika nchini Ufaransa.

Taarifa nyingine zimesema, De Bosque atachana rasmi na kazi ya ukocha wa timu ya taifa ya Hispania, baada ya kukamilisha taratibu za kikazi ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa ripoti na Julai 14.

Hofu ya Kushambuliwa na Wazawa Yaibuka Kenya.
Serengeti Boys Wapo Tayari Kwa Pambano La Kesho