Watoto wachanga wakike zaidi ya 10 wa jamii ya kimasai, wamenusurika kukeketwa katika kijiji cha Masaini , Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Watoto hao  walipangiwa kukeketwa katika kipindi cha Agosti 2017 hadi Februari 2018,wameokolewa katika hatua ya mwisho kabla ya kufanyiwa ukatili huo na shirika lisilo lakiserikali linalo jihusisha na masuala ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa makundi maalumu yakiwamo ya wanawake na Vijana TUSONGE.

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa mradi wa kupinga mila na desturi potofu zinazo pelekea ukatili wa kijinsia na ukeketaji, Joyce Kessy ameeleza kuwa watoto hao wachanga waliokolewa katika nyakati tofauti, “katika kipindi cha Disemba ndicho kipindi ambacho jamii ya wafugaji hufanya sherehe za ukeketaji na kipindi hicho ndicho tulifanikiwa kuwaokoa watoto hao, na sasa tumeweka makakti wa pamoja na maofisa Afya walioko katika maeneo hayo ili kukabiliana kila mzazi atakayempeleka mtotowake hospitali kwa ajili ya matibabu akaguliwe kama amekeketwa” aliongeza Kessy

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TUSONGE, Agnatha Rutazaa, aliiomba Serikali kuyaimarisha mabaraza ya usuluhishi yaliyoko ndani ya kata ilikuweza kutenda haki pindi wanapotoa maamuzi bila kuangalia uwezo wa mtu, na pamoja na hayo amesema katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 10, shirika la TUSONGE limeanza kutoa elimu kwa makundi ya vijana ili kuwa chachu ya mabadiliko ndani ya jamii katika kukemea masuala ya ukeketaji.

 

 

Chid Benz amuwakia Afande Sele, ‘tukikutana ni mimi na wewe’
Kusaga asema Fiesta itafanyika 'mwezi huu', aliongea na Rais

Comments

comments