Jumla ya watoto wachanga kumi wamethibitika kuambukizwa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19 muda mfupi baada ya kuzaliwa  katika hospitali moja iliyopo nchini Romania.

Kwa mujibu wa taarifa ya Deccan Herald, inasadikiwa kuwa watoto hao waliambikizwa virusi na wauguzi wa afya waliokuwa wanaendelea kuwatibu wagonjwa wa Covid 19.

”wauguziwalikuwa hawavai  ‘mask’ wakati wakuwahudumia watoto na siku ya jumanne nilisikia kuna kisa cha mgonjwa wa corona katika hospitali hii ” amesema mzazi mmoja

Hata hivyo Waziri wa Afya wa Romania Neru Tataru amesema kuwa watoto hao hawaonyeshi dalilizozote za Covid 19 na kuongeza kuwa wazazi wa watoto hao hawana maambukizi ya virusi hivyo.

Romania kumekuwa na kesi 4400 za  watu waliopata maambukiza ya virusi vya Corona huku kukiwa na vifo vya watu 180 waliokufa na ugonjwa huo.

 

Young Africans, GSM mambo BAM BAM
Serikali yazungumzia taarifa za wabunge 17 kukutwa na virusi vya corona – Kenya

Comments

comments