Meneja wa Manchester United, Erik ten Hag amefanya uamuzi wa kubaki na huduma ya beki wa kati Victor Lindelof baada ya kukoshwa na kiwango chake.

Sasa beki huyo wa kati raia wa Sweden atapewa ofa ya mkataba mpya baada ya kumalizia msimu huu katika kiwango bora kabisa cha ndani ya uwanja.

Mkataba wake wa sasa huko Old Trafford utafika tamati mwakani na Man Utd imeamua kukifanyia kazi kipengele cha kumwongezea mwaka mmoja zaidi kilichokuwa kimewekwa kwenye mkataba huo.

Lindelof alianzishwa kwenye mechi 12 za mwisho msimu huu baada ya Lisandro Martinez kuwa majeruhi na hivyo akimpiku Harry Maguire kwenye chaguo la mabeki katika kikosi hicho.

Lindelof, 28, alinaswa na Man United kutokea Benfica kwa ada ya Pauni 31 Milioni mwaka 2017 na ilionekana kama angefunguliwa mlangoni wa kutokea na kocha Ten Hag.

Man United inapiga hesabu za kumtupa nje ya timu nahodha wao Maguire na wapo kwenye mchakato wa kunasa huduma ya beki mwingine wa kati kutoka Napoli, Kim Min-jae.

Saba wapukutishwa Leicester City
Utatu mtakatifu kuibukia Newcastle Utd?