Mustakabali wa beki wa kati kutoka nchini England Christopher Lloyd “Mike” Smalling kuendelea kuwa mchazaji wa Man Utd upo shakani, kutokana na mipango inayosukwa huko Old Trafford kuelekea Januari 2017.

Gazeti la The Daily Express limeandika taarifa inayohusu mustakabali wa beki huyo aliyejiunga na Man Utd mwaka 2010 akitokea Fulham, ambapo limeeleza Jose Mourinho amedhamiria kumuondoa kikosini mwake.

Mpango wa kuuzwa kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 27, unahusishwa na mkakati wa kuwa sehemu ya kusalijiwa kwa beki kutoka nchini Sweden na klabu ya Benfica ya Ureno Victor Lindelof.

Ada ya usajili wa beki huyo inatajwa kuwa pauni milioni 37.8, lakini Man Utd hawapo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa na badala yake wamejipanga kumjumuisha Smalling kwenye dili hilo.

Mpango huo unadhihirisha wazi kuwa, mabeki Phil Jones na Marcos Rojo wataendelea kuwa chaguo la kwanza la Mourinho kufuatia kuumia kwa Bailly huku wakisubiri huduma ya Lindelof.

Bartomeu: Messi Anajua FC Barcelona Ni Klabu Ya Aina Gani
Video: Lema augua ghafla selo, Mauaji yaliyotikisa 2016...