Klabu ya Tottenham imekamilisha usajili wa kiungo kutoka nchini Kenya Victor Wanyama kwa ada ya uhamisho ya Pauni million 11 akitokea Southampton.

Wanayama amejiunga na Spurs kwa ushawishi mkubwa, wa aliyekua meneja wake Mauricio Pochettino, ambaye alimsajili mwaka 2013 akitokea kwenye klabu ya Celtic ya Scotland na kujiunga na Southampton kwa ada ya Pauni milioni 12.5.

Kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuwekea kaskazini mwa jijini London hadi mwaka 2021, na inaamiwa atakuwa mmoja wa wachezaji watakaoiwezesha Spurs kufanya vyema katika ligi ya nchini England pamoja na michuano ya barani Ulaya kwa msimu ujao.

Pochettino, alionyesha dhamira ya kutaka kumsajili Wanyama tangu msimu uliopita, lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na msimamo uliokua umewekwa na viongozi wa Southapton.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, anakua mchezaji wa kwanza kusajiwa na Spurs katika kipindi hiki cha kujiandaa na msimu wa 2016-17.

LHRC Kutekeleza Majukumu Kiufasaha Zaidi
Mbunge CCM ataka Mbwa, Michango ya Misiba, Sadaka, harusi, kulipiwa kodi