Kiungo kutoka nchini Kenya, Victor Wanyama ameugomea uongozi wa klabu ya Southampton katika suala la kusaini mkataba mpya, kwa kushinikiza kuondoka klabuni hapo.

Wanyama amefanya maamuzi hayo, huku ikifahamika aliyekua meneja wa The Saint, Mauricio Pochettino anahitaji kuona akikamilisha harakati za kumsajili wakati wa dirisha la usajili ili wawe wote Tottenham Hotspurs.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu ya Southampton ambayo ilimsajili akitokea Celtic mwaka 2013, kwa ada ya Pauni milioni 12.5.

Kutokana na hatua hiyo uongozi wa The Saint, kwa sasa unasubiri ofa yoyote itakayomlenga kiungo huyo na tayari wameshaweka wazi thamani yake kwa kutaja kiasi cha Pauni milioni 25.

Klabu bingwa nchini England Leicester City, pia inatajwa kuwa katika mlolongo wa kutuma ofa St Mary’s, ili kuangalia uwezekano wa kumsajili Wanyama.

Wanyama, anapigiwa upatu wa kusajiliwa huko King Power Stadium, ili kuwa sehemu ya mbadala wa kiungo kutoka nchini Ufaransa N’Golo Kante ambaye amegoma kusaini mkataba mpya.

Majaliwa atoa onyo kali, akazia nguvu msako wa wala Rushwa, Mafisadi
Leicester City Waanza Kuuza Wachezaji Wao